Viongozi wa afya nchini Drc wamethibitisha kutokea kesi nane za maambukizo ya Ebola katika jimbo la kivu kaskazini , shirika la afya ulimwenguni WHO limesema jumatano.
Huu ni mlipuko mpya nchini humo. Katika kesi hizo nane, kuna vifo sita, imesema hayo ofisi ya WHO kwa ajili ya afrika kwa njia ya ukurasa wake wa twitter.
Takriban watu 573 walioambukizwa virusi hivyo wametambuliwa. Kumekuwa na kuibuka tena kwa maambukizi ya Ebola nchini humo mwaka huu.
Mlipuko wa awali wa Ebola nchini Drc ulitangazwa umekwisha mwezi Mei mwaka huu, ulisababisha vifo vya watu 2,287 tangu mwezi Agosti 2018