Wajukuu zake walimwagia sifa kemkem kiongozi huyo wa zamani wa Kenya, aliyefariki Jumanne ya Februari 4, 2020 akiwa na umri wa miaka 95 wakisema kuwa alikuwa mchapa kazi na mkweli.
Wajukuu zake wa kike walisema alikuwa anawaambia siku zote wamweke Mungu mbele kuliko kitu chochote na wala wasichukulie vitu juu juu.
“Msiwategemee binadamu kwani siku zote watakuangusha, siku zote imani yako iweke kwa Mungu,” mmoja wa wajukuu zake wa kike, Laila Cherobon amesema.
Clint Kiprono Moi, mjukuu wake wa kiume, alisema alikuwa na hisia mchanganyiko kufuatia kifo cha Moi.
Kwa upendo anakumbuka kuwa alipokuwa mdogo zaidi, jina lake la ukoo lilikuwa linafanana na la rais, wakati watu walikuwa mara kwa mara wanauliza : “Moi wa Uganda ni nani.?”
Daktari David Silverstein, ambaye alikuwa daktari wake binafsi Moi, anaeleza kuwa kulikuwa na mahusiano makubwa zaidi kuliko yale ya daktari na mgonjwa wake, wakati akikumbuka mambo mengi yaliyo katika kumbukumbu yake waliokuwa wakijadili.
Anasema walikutana mwaka 1970 na kubakia kuwa marafiki hadi mwisho wa uhai wake.
“Moi alishiriki katika matukio muhimu ya maisha yangu… sikukuu ya kuzaliwa ya mtoto wangu na ndoa ya Channa,” aliwaambia waliohudhuria katika ibada hiyo kwenye viwanja vya Kabarak.
Aligusia kuwa mbali na kuwa Moi alipenda nyama, pia alipenda kunywa mvinyo pamoja naye na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Charles Njonjo, ambaye alisheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa mwezi uliopita alipofikisha miaka 100.