Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 21:32

Rais Kenyatta na mkewe wamewaongoza wakenya kuuaga mwili wa Moi


Daniel Arap Moi, Rais wa pili wa Kenya

Umati wa wakazi wa Kenya Jumamosi asubuhi walijipanga kwenye mitaa ya Nairobi wakisubiri kuingia majengo ya Bunge la Kenya kuuaga mwili wa Raiswao wa zamani nchini humo, Daniel Arap Moi aliyefariki Jumanne ya Februari 4 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret Kenyatta walikuwa watu wa kwanza siku ya Jumamosi kuuaga mwili wa Rais wa pili wa Kenya, Daniel Arap Moi kwenye majengo ya bunge katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Wakati huo huo umati wa wakazi wa Kenya Jumamosi asubuhi walijipanga kwenye mitaa ya Nairobi wakisubiri kuingia majengo ya Bunge la Kenya kuuaga mwili wa Rais wao wa zamani nchini humo, Daniel Arap Moi aliyefariki Jumanne ya Februari 4 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95.

Rais Kenyatta akiwa Ikulu ya Nairobi kabla ya kuelekea bungeni alitoa hotuba ya moja kwa moja kwenye televisheni akitamka maneno mazuri yaliyomsifu rais huyo wa zamani kama baba wa taifa la kenya.

Rais Daniel Arap Moi enzi za uhai wake akila kiapo cha kuongoza taifa la Kenya
Rais Daniel Arap Moi enzi za uhai wake akila kiapo cha kuongoza taifa la Kenya

Daniel Arap Moi alihudumu kama Rais wa Kenya kutoka mwaka 1978 hadi 2002. Alichukua urais kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta kilichotokea Agosti 22 mwaka 1978. Moi atazikwa Jumatano ya Februari 12 katika makazi yake huko Kabarak nchini Kenya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG