Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 11:49

Mkapa kuzikwa Mtwara na kuagwa kitaifa wiki ijayo


Hayati Rais Mkapa
Hayati Rais Mkapa

Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa aliyefariki Alhamisi akiwa na umbra wa miaka 81 atazikwa kijijini kwake Lupaso, wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara, Kusini mwa Tanzania.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Ijumaa kuanzia siku ya Jumapili, mwili wa marehemu utaletwa uwanja wa uhuru mjini Dar es Salaam kwa aijli ya kuagwa. Programu hiyo ya kuuaga mwili wa marehemu itaendelea kwa siku tatu (Julai 26-28).

Kanisa Katoliki limeandaa misa ambayo wakazi wa Dar es Salaam na nje ya mji huo watapata fursa ya kuuaga mwili wa marehemu siku nzima ya Jumapili hadi Jumatatu.

Mwili wa marehemu utaagwa kitaifa siku ya Jumanne Julai 28 na viongozi mbalimbali watahudhuria. Baada ya programu hiyo mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda wilayani Masasi na kuagwa na wazazi wa eneo hilo.

Mwili wa marehemu utatua katika uwanja wa ndege wa Nachingwea na kutoa fursa kwa wakazi wa eneo hilo kuaga mwili wa marehemu.

Mzee Mkapa alizaliwa Novemba 1938, Mkoa wa Mtwara kusini mwa Tanzania, na aliliongoza taifa hilo kwa mihula miwili toka mwaka 1995 mpaka 2005.

XS
SM
MD
LG