Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 11:53

Harris akamilisha ziara ya Vietnam


Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kuondoka Vietnam akirejea Marekani baada ya kukamilisha ziara ya Asia, Hanoi, Vietnam, Agosti 26, 2021. REUTERS/Evelyn Hockstein/Pool

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ameondoka Vietnam Alhamisi akiwa anakamilisha ziara yake ya kusini mashariki mwa Asia.

Harris alikutana na maafisa wa juu wa Singapore kabla ya kutembelea Vietnam katika hatua ya kuimarisha ushirika wa Marekani katika eneo hilo kupambana na ushawishi wa China.

“Mimi ni Makamu wa Rais wa kwanza kutembelea Vietnam tangu uhusiano wa kidiplomasia ulipoanzishwa mwaka 1995, ninaamini kwamba safari hii inatoa ishara ya mwanzo ya ukurasa mpya katika uhusiano baina ya Marekani na Vietnam.”

Aligusia idadi ya mikataba ya Marekani ikiwemo ushirikiano wa ulinzi wa mitandao na msaada wa kupambana na virusi vya Corona nchini Vietnam, ambayo inapambana na wimbi jipya la virusi na kiwango kidogo cha chanjo.

Harris amesema amezungumzia kuhusu suala la ukiukwaji wa haki za binadamu na viongozi wa Vietnam lakini hakutoa ishara zozote kama mazungumzo hayo yamezaa matunda.

Vietnam imekosolewa kwa masharti ya kuzuia uhuru wa kuzungumza na waandishi wa habari pamoja na ukandamizaji kwa watu wenye mtazamo wa upinzani wa kisiasa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG