Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 10:59

Maafa yaongezeka Haiti kufuatia tetemeko la ardhi


Mabaki ya nyumba zilizoporomoka Haiti baada ya tetemeko
Mabaki ya nyumba zilizoporomoka Haiti baada ya tetemeko

Maafisa wa Haiti wamesema Jumapili kwamba idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi mwishoni mwa wiki imefikia 700 huku wengine zaidi ya 1,800 wakisemekana kuachwa na majeraha.

Tetemeko hilo lilitokea Jumamosi karibu na mji wa Petit Trou de Nippes, takriban kilomita 125 magharibi mwa mji mkuu wa Port au Prince likisemekana kuwa na kina cha kilomita 10 chini ya ardhi kulingana na wataalamu wa jeolojia.

Waziri mkuu mpya Ariel Henry aliyechukua madaraka wiki 3 zilizopita baada ya kuukawa kwa rais Jovenel Moise amesema kuwa serikali imepeleka misaada kwenye maeneo yalioathiriwa.

Wakati akizungumza na shirika la habari la AP, kiongozi huyo amesema kuwa nia yao ni kuokoa maisha ya watu wengi iwezekanavyo. Mji wa Les Cayes ambao ni mkubwa zaidi karibu na kitovu cha tetemeko hilo umeshuhudia majengo yaliyo poromoka na hospitali zilizojaa majeruhi.

Rais wa Marekani Joe Biden pamoja na makamu wake Kamala Harris Jumamosi walifahamishwa kuhusu hali halisi nchini Haiti baada ya janga hilo kutokea

XS
SM
MD
LG