Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:32

Watu 50 wakiwemo watoto 7 wapoteza maisha Kenya


Basi lililoharibika baada ya kupinduka kwenye ajali ya Kericho, magharibi ya Kenya, Octoba 10, 2018.
Basi lililoharibika baada ya kupinduka kwenye ajali ya Kericho, magharibi ya Kenya, Octoba 10, 2018.

Watu wasio pungua 50 wameuwawa baada ya basi kuacha njia na kupinduka katika mteremko mkali na kugonga magharibi mwa Kenya, afisa mmoja wa usalama amesema Jumatano.

Ajali hiyo imetokea saa kumi alfajiri na katika ya wale waliopoteza maisha saba ni watoto, ameongeza. Paa la basi hilo lilifumuka wakati wa ajali hiyo.

Kiasi cha manusura 15 kutoka katika basi hilo ambalo lilikuwa linaelekea mjini Nairobi, upande wa magharibi wa mji wa Kakamega, wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Kericho, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Rift Valley Francis Munyambu amesema.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kericho James Mugera amesema dreva alishindwa kulizuia gari baada ya kuanza kushuka katika mteremko kabla ya gari hilo kugonga.

Mtu mmoja aliyenusurika ambaye alipelekwa hospitali ana kumbuka ajali hiyo ya siku ya Jumanne, akisema “ gari hilo lilikuwa lina yumba na kupinda pinda, ndipo nilipokuja kugundua kwamba lilikuwa linawatupa abiria nje na miili ilikuwa imesambaa pande zote."

Wakati huohuo Mkuu wa polisi wa usalama barabarani katika kaunti ya Rift Valley, Zero Arome anasema kuna ulazima serikali, polisi, madereva na wasafiri wawajibike ili kuzuiya ajali hizo za barabarani zinazosababisha maafa mengi.

Kamanda Arome amewalaumu madereva wa bus kwa kile anachosema “ wanakiuka sheria za usafiri wa barabarani kwa kuendesha gari kwa mwendo kasi.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa watu 3,000 hufariki kila mwaka katika ajali za barabarani nchini Kenya, lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) limekariri hisabu ya vifo kuwa ni 12,000.

Mwaka 2016, trela la mafuta lililipuka na kusababisha moto mkubwa baada ya ajali, kwenye barabara ya kutoka Kericho kuelekea Nairobi, na kuuwa watu 40.

XS
SM
MD
LG