Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:39

Ajali Kenya yaua wanne


Watu wanne wamepoteza maisha Jumapili asubuhi katika ajali ya gari iliyaohusisha basi la abiria na lori katika barabara ya Garrissa -Wajir nchini Kenya.

Ajali hiyo wakati basi lilipo ligonga lori lililokuwa limesimama majira ya saa saba usiku.

Polisi wamesema abiria wengine 10 wamejeruhiwa vibaya sana katika ajali hiyo na wamelazwa hospitalini.

Mkuu wa Polisi katika eneo la Wajir Stephen Ngetich amesema kuwa wanachunguza ni namna gani na kwa nini ajali hiyo ilitokea.

Tunachofahamu ajali hii ilitokea usiku na bado hatujaweza kujua mazingira yaliyopelekea ajali hiyo kutokea.

Basi hilo lilikuwa likielekea Wajir limebeba abiria 50 wakati ajali inatokea kwenye eneo la Habaswen.

Hii ni ajali nyingine ya hivi karibuni kutokea nchini pamoja na kuwepo kampeni ya kuzuia kuendelea kwa janga hili.

Makumi ya watu waliuwawa tangia mwanzoni mwa mwaka huu katika muelekeo ambao unaongopesha. Mnamo mwezi Disemba 2017 peke yake, Zaidi ya watu 360 waliuwawa katika ajali tofauti nchini Kenya.

Hili lilipelekea serikali kupiga marufuku safari za usiku kwa magari yote ya umma ikiwa ni sehemu ya juhudi ya kuzuia ajali hizo za barabarani

XS
SM
MD
LG