Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:46

Vikosi vya usalama Kenya vyafanikiwa kuwatimua al-Shabaab


Magaidi wa kikundi cha al-Shabaab
Magaidi wa kikundi cha al-Shabaab

Magaidi wanaoshukiwa kuwa ni kikundi cha al-Shabaab wameshambulia msafara wa mabasi yaliyokuwa yanatokea Lamu kuelekea Malindi na Mombasa.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Mwenda Njoka shambulizi hilo lilitokea majira ya saa tano asubuhi Jumamosi.

Ameeleza kuwa kulikuwa na utupianaji wa risasi kati ya kikosi cha usalama kilichokuwa kinayasindikiza mabasi hayo na washambuliaji ambapo raia mmoja alipigwa risasi na kuuwawa na baadhi ya polisi kujeruhiwa.

Gari mbili za polisi ziliharibiwa wakati wa mapambano hayo ya bunduki. Hata hivyo haijaweza kujulikana ni washambuliaji wangapi waliuwawa au kujeruhiwa wakati wa tukio hilo lilitokea eneo la Nyongoro kati ya kitongoji cha Gamba na Simba nchini Kenya.

Mara baada ya shambulizi hilo , msafara wa maafisa wa usalama vikiwemo vikosi vya anga na ardhini vilipelekwa kutoka kituo cha operesheni maalum cha Boni.

Hatua za mara moja zilizochukuliwa na timu ya usalama iliwezesha magari hayo kuvuka eneo la tukio la shambulio kwa usalama na bila majeruhi zaidi. Hadi mchana huu, operesheni ya kuhakikisha usalama katika eneo hilo inaendelea.

XS
SM
MD
LG