Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 09:07

Ajali ya barabara ya Nairobi-Nakuru yaua 3


Eneo la ajali Kenya

Watu watatu wamethibitishwa kuuwawa katika ajali mbaya ya barabarani Jumapili asubuhi karibu na eneo la Marula huko Naivasha kwenye barabara kuu ya Nairobi - Nakuru nchini Kenya.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa Dereva wa kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Wawakilishi Kaunti ya Laikipia Peter Thomi ni kati ya wale waliouwawa katika ajali hiyo na polisi wamethibitisha hilo.

Mwakilishi huyo, na abiria kadhaa pamoja madereva wa gari nyingine wamejeruhiwa na wamelazwa katika hospitali iliyoko karibu na eneo hilo ambapo ajali ilitokea.

Ajali hiyo yenye kushangaza ili husisha magari matano yakiwemo mabasi mawili na kusababisha msongamano mkubwa katika barabara hiyo kwenye eneo la ajali.

Jeshi la polisi nchini Kenya limewatahadharisha madereva kuwa waangalifu zaidi wakati huu wa majira ya mvua kwani kutokana na ukungu barabara zina kiza sana.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG