Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 02:47

Hali ya hewa imezorotesha juhudi za uokoaji katika ajali ya majini Hungary


Boti za ukoaji zikijiandaa kuanza shughuli za uokozi baada ya boti kuzama chini ya daraja la Margaret Hungary, Mei 30, 2019.
Boti za ukoaji zikijiandaa kuanza shughuli za uokozi baada ya boti kuzama chini ya daraja la Margaret Hungary, Mei 30, 2019.

Waokoaji wanafanya kazi usiku na mchana tangu meli kubwa na boti ya watalii kugongana Jumatano usiku katika Mto Danube, Hungary na wanasema mvua kubwa, upepo mkali na maji yanayotembea kwa kasi yamekuwa kizuizi katika juhudi za uokoaji.

Pia kumekuwa na taarifa ya kuwa juhudi za kuopoa miili ya wale waliokufa zimekabiliwa na changamoto ya kuona maiti hizo kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inaendelea katika eneo hilo la mto Danube.

Vyanzo vya habari Budapest vimeeleza kuwa kutokana na mshituko mkubwa ambao uliwakumba wasafiri katika boti, haijafahamika kwamba wahanga wa ajali hiyo waliweza kupata muda wa kuvaa life jacket.

Taarifa kutoka Budapest zinaeleza kuwa watu 7 wamefariki na wengine 21 hawajulikani walipo. Wasafiri wote, ukitoa wawili kati yao, walikuwa watalii wa Korea Kusini.

Ndugu wa mtalii wa Korea Kusini aliyetoweka baada ya meli kubwa kugongana na boti yao ya utalii huko Hungary wanatarajiwa kuwasili Hungary Ijumaa.

Taarifa kutoka Budapest zinasema kuwa wakati ajali hiyo inatokea kulikuwa na mvua kubwa inayonyesha na hivyo kunauwezekano kwamba manahodha wa vyombo hivyo hawakuweza kutambua uwepo wa chombo kingine karibu yao. Hata hivyo vyombo husika vinaendelea na uchunguzi.

Hata hivyo wataalamu wanasema kuwa vyombo hivyo vina chombo ambacho kinaweza kutoa tahadhari kwa nahodha juu ya uwepo wa vyombo vingine vya majini vinapokuwa vimekaribiana.

Polisi wamesema wanamshikilia nahodha wa meli ya Viking ambaye ni raia wa Ukraine akishukiwa kuhusika na kuhatarisha usafiri wa majini katika ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG