Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:41

Ajali ya boti yauwa watu 30 Uganda


Shughuli za uokoaji zikiendelea katika fukwe ya Ziwa baada ya boti kuzama nje kidogo ya eneo la Wilaya ya Mukono, Uganda, Nov. 25, 2018.
Shughuli za uokoaji zikiendelea katika fukwe ya Ziwa baada ya boti kuzama nje kidogo ya eneo la Wilaya ya Mukono, Uganda, Nov. 25, 2018.

Watu 30 wamefariki nchini Uganda katika ajali ya boti Jumapili iliyotokea katika eneo la Ziwa Victoria.

Polisi nchini humo wamethibitisha ajali hiyo na wamesema shughuli za uokoaji bado zinaendelea.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa msimamizi wa zoezi hilo la uokoaji Kamanda wa Polisi Asuman Mugenyi amesema kuna uwezekano mdogo wa kuwapata wanusurika hao waliokuwa wakielekea kwenye sherehe.

Vyanzo hivyo vimeripoti chombo hicho kilikuwa kikisafirisha zaidi ya watu 120 kwenda Mpatta Wilaya ya Mukono, ambacho ni kisiwa kimojawapo katika Ziwa Victoria.

Vyanzo vingine vya habari vimeeleza kuwa Prince David Wasajja, ndugu wa mfalme wa Buganda, Uganda Kabaka Ronald Mutebi alikuwa pia kwenye boti hiyo lakini aliokolewa.

Vyombo vya habari nchini Uganda vinaripoti kuwa mwanamuziki Iryn Namubiru amenusurika katika ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG