Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 12:27

Habari mpya ya Vita vya Ukraine: Mapambano makali yaripotiwa mashariki mwa Ukraine


Mwanajeshi wa Ukraine wa kikosi cha 3rd Assault Brigade akifyatua kombora milimita 122 kuelekea eneo la Russia katika mstari wa mbele wa mapambano, karibu na Bakhmut, mkoa wa Donetsk, Ukraine, Julai 2, 2023.
Mwanajeshi wa Ukraine wa kikosi cha 3rd Assault Brigade akifyatua kombora milimita 122 kuelekea eneo la Russia katika mstari wa mbele wa mapambano, karibu na Bakhmut, mkoa wa Donetsk, Ukraine, Julai 2, 2023.

Naibu Waziri wa Ulinzi Hanna Maliar alisema kupitia ujumbe wa Telegram kuwa wanajeshi wa Ukraine walikuwa wanasonga mbele katika eneo la Bakhmut upande wa mashariki, wakati Russia ilikuwa ikiendelea kushambulia huko Lyman, Adviivka na Mariinka.

Maliar alisema kulikuwa na “mapigano makali yanaendelea” katika maeneo hayo.

Mafanikio mengi ya Ukraine yalikuwa yamepatikana upande wa kusini mwa nchi, Maliar alisema, huku eneo la kilomita za mraba 28 zikikombolewa katika kipindi cha wiki iliyopita.

Aliongeza kuwa jeshi la Ukraine lilikuwa linafanya operesheni za mashambulizi mbalimbali katika maeneo ya Melitopol na Berdyansk.

Ukraine ilianza kujibu mashambulizi mapema mwezi Juni ikijitahidi kuyakomboa maeneo yaliyovamiwa na Russia tangu kuanza kwa uvamizi wa Ukraine mwezi Februari 2022.

Uhalifu Unaotokana na Uvamizi

Kituo kipya kilifunguliwa Jumatatu huko The Hague kikijikita katika kuchunguza na kukusanya ushahidi kuhusu uwezekano wa kuwepo uhalifu wa Russia katika uvamizi wake wa Ukraine kuhusiana na vita hivyo.

Kituo cha Kimataifa cha Mashtaka ya uhalifu wa uvamizi (ICPA) kimefunguliwa ili kifanye kazi sambamba na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

ICC inaweza kufungua mashtaka dhidi ya uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari, lakini haina mamlaka ya uhalifu wa uvamizi.

Wizara ya Sheria ya Marekani ilisema mwezi uliopita kuwa kituo kipya cha ICPA “kitakuwa na jukumu muhimu katika mazingira hayo kufungua mashtaka ya uhalifu wa uvamizi wa uharibifu wa kivita uliofanywa huko Ukraine.”

Ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wao, ICPA itachunguza jukumu la maafisa wa Russia katika vita hivyo.

Russia imekanusha kuwalenga raia au kuhusika na uhalifu wa kivita.

Baadhi ya taarifa zilizomo katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AF, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG