Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 02:19

Vita vya Ukraine: Mjumbe wa Papa aenda Moscow


Papa Francis akisalimiana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipowasili Vatican, tarehe 13 Mei Picha na Kitini / VATICAN MEDIA / AFP.
Papa Francis akisalimiana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipowasili Vatican, tarehe 13 Mei Picha na Kitini / VATICAN MEDIA / AFP.

Mjumbe wa amani wa Papa Francis, Kadinali Matteo Zuppi amesafiri kwenda Moscow wiki kadhaa baada ya kutembelea Kyiv, na Vatican imesema kuwa anatafuta "suluhisho la hali mbaya ya sasa" ya kivita nchini Ukraine.

Maafisa wa Ukraine wamesema Jumatano kuwa shambulizi la kombora la Russia katika mji wa Kramatorsk limeua takriban watu tisa na kuwajeruhi wengine zaidi ya 50.

Huduma za dharura zilichapisha picha za timu za uokoaji zikiwatafuta waathirika katika vifusi yakiwemo vya mgahawa.

Kramatorsk iko magharibi mwa eneo ambalo mapigano yanafanyika katika mkoa wa Donetsk uliopo mashariki mwa Ukraine.

Mwezi Aprili mwaka 2022, shambulizi la Russia katika kituo cha reli kilichopo eneo la jiji liliua watu 63.

Ukraine pia iliripoti shambulizi la kombora la Russia la Jumanne huko Kremenchuk, ambalo limefanyika mwaka mmoja baada ya shambulio la Russia lililouwa watu takribani 20 kwenye shopping mall.

Baadhi ya taarifa hizi zinatoka katika mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG