Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 18:28

Biden kuhudhuria mkutano wa NATO wiki ijayo


Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden.

Rais wa Marekani Joe Biden anaondoka wiki ijayo kwa ziara  ya siku tano ya mataifa matatu barani Ulaya, ikulu ya Marekani ilisema Jumapili.

Kituo chake kikuu kitakuwa ni mkutano wa kila mwaka wa NATO mjini Vilnius, Lithuania, ambapo viongozi wa nchi za Magharibi wanapanga kujadili juhudi za hivi punde, za kuisaidia katika vita vya Ukraine dhidi ya Russia.

Biden, kwanza ataelekea mjini London Jumapili ijayo, katika safari itakayoanza Julai 9 hadi 13, ambapo kwa siku mbili, anapanga kukutana na Mfalme Charles na Waziri Mkuu Rishi Sunak, katika kile ikulu ya Marekani inasema ni juhudi za kuimarisha zaidi, uhusiano wa karibu kati ya mataifa hayo mawili."

Nchi wanachama wa NATO, zikiongozwa na Marekani, zimetuma mabilioni ya dola za kugharamia ununuzi wa silaha nchini Ukraine, lakini mashambulizi ya anga ya Russia yameendelea kusababisha vifo vya darzani za raia wa Ukraine, hata ingawa majeshi ya Kyiv yamharibu mamia ya makombora ya Russia. Yale ambayo yametua yameonekana kuharibu, kuua watu na kuharibu majengo yao ya makazi.

Baada ya mkutano wa kilele wa NATO, Biden ataelekea Helsinki, mji mkuu wa Finland, kuadhimisha hatua ya hivi karibuni, ya Finland kujiunga na muungano huo wa kijeshi, ulioundwa baada ya Vita vya pili vya dunia, na kukutana na viongozi wa mataifa ya ukanda wa Nordic.

Forum

XS
SM
MD
LG