Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 21:00

Waandamanaji wachoma Kurani nje ya msikiti mjini Stockholm


Maandamano yalifanyika mjini Istanbul, Uturuki kufuatia kitendo cha kuchoma Kurani mjini Stockholm, Januari 29, 2023.

Mwanaume mmoja alichukua Kurani na kuichoma nje ya msikiti mjini kati Stockholm leo Jumatano baada ya polisi wa Sweden kuruhusu maandamano, tukio ambalo linaweza kuikasirisha Uturuki wakati Sweden inaomba kujiunga na muungano wa NATO.

Polisi baadaye walimshtaki mwanaume huyo kwa uchochezi dhidi ya kundi la kikabila au la taifa.

Msururu wa maandamano nchini Sweden dhidi ya Uislamu na kwa ajili ya haki za Wakurdi yameikasirisha Ankara, ambayo Sweden inahitaji uungaji mkono wake ili kujiunga rasmi na NATO.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan amelaani kitendo hicho kwenye Twitter, akiongeza kuwa ni jambo lisilokubalika kuruhusu maandamano dhidi ya Uislamu kwa madai ya uhuru wa kujieleza.

Takriban watu 200 waliokuwa wanatazama maandamano hayo wameshuhudia mmoja wa waandalizi wawili akichukua kurasa za nakala ya Kurani na kuzikanyaga na viatu vyake kabla ya kuweka ndani yake nyama ya nguruwe na kuchoma moto kitabu hicho.

Baadhi ya waliokuwa kwenye eneo la tukio walipaza sauti wakisema “Mungu ni mkubwa” kwa Kiarabu kupinga kitendo hicho cha kuchoma Kurani, na mtu moja alikamatwa na polisi baada ya kujaribu kurusha jiwe.

Forum

XS
SM
MD
LG