Shirika hilo linapanga kupunguza idadi ya safari kuingia Lagos kutoka safari 11 hadi 7, kuanzia katikati mwa mwezi Agosti.
Limesema kwamba kiasi cha dola milioni 85 zimekwama nchini humo kuanzia mwezi July na kiwango cha pesa kimekuwa kikiongezeka kwa dola milioni 10 kila mwezi.
Wataalam wa sekta hiyo wanasema huenda mashirika mengine ya ndege yatafuata mkondo huo iwapo hatua hazitachukuliwa kukabiliana na uhaba wa dola na kutatua changamoto ambazo mashirika ya ndege yanapitia.
Facebook Forum