Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:23

Afisi ya UN ya kupambana na ugaidi inahimiza ushirikiano katika kupambana na ugaidi nchini Nigeria


Askari wa kulinda usalama wapiga doria katika kijiji cha Kenam jimbo la Plateau nchini Nigeria, baada ya nyumba za wakazi kuchomwa na majambazi, April 12, 2022. Picha ya AFP
Askari wa kulinda usalama wapiga doria katika kijiji cha Kenam jimbo la Plateau nchini Nigeria, baada ya nyumba za wakazi kuchomwa na majambazi, April 12, 2022. Picha ya AFP

Afisi ya Umoja wa mataifa ya kupambana na ugaidi inasema kuna umuhimu wa kuweka msingi imara wa ushirikiano kati ya mashirika ya serikali ya Nigeria katika usimamizi wa taarifa zinazohusiana na ugaidi na magaidi.

Afisi hiyo imebaini hayo katika mkutano maalum ambao unafanyika Abuja Nigeria unaosadikiwa utakuwa na uwezo wa kulisaidia taifa hilo kufuatilia harakati za magaidi katika eneo lake.

Kukithiri kwa harakati za kigaidi nchini Nigeria katika siku za karibuni kumezua hali ya sintofahamu miongoni wa raia wanaoishi kwa hofu licha ya juhudi za serekali kukabiliana na tishio hilo.

Katika mkutano ulioandaliwa na afisi ya Umoja wa mataifa ya kupambana na ugaidi mjini Abuja, Umoja wa mataifa unapanga kupata ushirikiano wa mashirika husika ya serekali katika usimamizi wa habari ambazo zitasaidia kutambua na kupambana na ugaidi duniani kote.

Marguerie Carpenta wa Afisi ya Umoja wa mataifa ya kupambana na ugaidi anasema kuna mtindo wa kawaida wa tabia ya kigaidi kwa kutumia sekta ya usafiri wa anga duniani kote.

Licha ya tishio la maisha na mali ya raia kutokana na ugaidi, baadhi ya viongozi wakijadi waliojenga urafiki na magaidi, wamekutwa na hatia ya kushirikiana na majambazi wanaojulikana kuhatarisha maisha na kuwaua watu hata kuwateua kuwa machifu katika eneo lao katika jamii nyingi za kaskazini mwa Nigeria.

Gavana wa jimbo la Zamfara Bello Matawale ambaye hivi karibuni aliwatimua viongozi wawili wakijadi kwa kushirikiana na magaidi, amemfukuza Aliyu Mafara Amri wa Birni Yandoto kwa kumteua kiongozi wa majambazi Ado Alero kama chifu wa kabila la Fulani katika himaya yake.

Mchambuzi wa masuala ya umma na mwanahabari Babajide Otitoju anasema mtazamo wa viongozi hawa wajadi unaweza kuwakatisha tamaa wanajeshi wanao hatarisha maisha yao kupambana na magaidi.

Ripoti hii imeandaliwa na Collins Atohengbe kutoka Lagos

XS
SM
MD
LG