Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 12:52

Maseneta Nigeria washinikiza Rais Buhari kufunguliwa mashitaka

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Maseneta wa upinzani nchini Nigeria walishinikiza Rais Muhammadu Buhari kukabiliwa na mashtaka, miezi 10 kabla ya kumalizika kwa muhula wake wa pili madarakani, kutokana na kuenea kwa matatizo ya usalama nchini humo, kiongozi wa walio wachache katika Seneti alisema Jumatano.

Raia wa Nigeria wataenda kupiga kura Februari 2023 kumchagua rais mpya katika kura yenye ushindani mkali ambapo usalama na hali ya uchumi itakuwa masuala makuu.

Katika kikao cha faragha cha Seneti, Maseneta wa chama cha People's Democratic Party (PDP) walijaribu kuwasilisha hoja iliyompa Buhari muda wa wiki sita kuboresha usalama wa nchi la sivyo atakabiliwa na mashtaka, Seneta Philip Aduda alisema.

XS
SM
MD
LG