Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:17

Jeshi la Nigeria lampata msichana wa shule ya Chibok miaka minane baada ya kutekwa nyara


Mmoja wa wasichana 82 wa shule ya Chibok akumbatiana na wazazi wake mjini Abuja baada ya kuachiwa huru, May 20, 2017. Picha ya Reuters
Mmoja wa wasichana 82 wa shule ya Chibok akumbatiana na wazazi wake mjini Abuja baada ya kuachiwa huru, May 20, 2017. Picha ya Reuters

Jeshi la Nigeria limempata mmoja wa wasichana wa shule ya kijiji cha Chibok aliyekuwa ametekwa nyara na kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram miaka minane iliyopita, maafisa wa jeshi wamesema Jumatano.

Msichana huyo alikuwa miongoni mwa wasichana wa shule 276 wenye umri wa kati ya miaka 12 na 17 ambao walitekwa nyara kwenye shule yao katika kijiji cha Chibok, kaskazini mwashariki mwa Nigeria mwaka wa 2014.

Kutekwa nyara kwao kulichochea kampeni ya kimataifa chini ya hashtag “BringBackOurgirls.”

Christopher Musa, kamanda wa wanajeshi katika eneo hilo, alimtambulisha Ruth Bitrus, mwenye umri wa miaka 24, akiwa na mtoto wake wa kiume wa miaka miwili kwa waandishi wa habari mbele ya kambi ya kijeshi.

“Leo tunaye miongoni mwetu mmoja wa wasichana wa Chibok, ni msichana wa tatu aliyepatikana ndani ya miezi miwili,” Musa amesema kwenye hafla ya kumpokea msichana huyo.

Lakini hakusema lini Bitrus alipatikana.

Inaelezwa kwamba mwanamke huyo, ambaye alikuwa na umri wa miaka 16 alipotekwa nyara, alitoroka usiku na kutembea kwa siku tatu msituni kabla ya kufika kwenye mji wa Bama na kuwakaribia wanajeshi.

XS
SM
MD
LG