“Kulikuwa abiria 16 ndani ya boti wakati ajali ilipotokea Ijumaa usiku,” Ibrahim Farinloye wa idara ya kitaifa ya dharura (NEMA) ameiambia AFP.
Maiti mbili zilipatikana baada ya mkasa huo Jumamosi, amesema.
Amesema miili 11 iliopolewa Jana Jumapili.
“Kujumuisha na hiyo, jumla ya miili 15 imeopolewa.”
Farinloye amesema abiria mmoja ametoweka.
Mamlaka ya Lagos ya usafiri wa baharini (LASWA) pia imethibitisha vifo hivyo.