Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 01:00

Dhoruba kubwa wikiendi ya Krismas yasitisha usafiri Marekani


Msongamano wa magari uliosababishwa na hali mbaya ya hewa Marekani

Kipande cha maili 70 sawa na kilomita 112 cha barabara kuu eneo la mashariki kwenye barabara kuu namba 80 kilifungwa hadi Jumatatu kutoka eneo la Colfax huko California kupitia eneo la ziwa Tahoe hadi jimbo la Nevada nchini Marekani

Dhoruba kubwa ya wikiendi ya Krismas ilisababisha umeme kukatika na kufungwa kwa barabara kuu kufuatia theluji iliyoshuka katika milima ya kaskazini mwa California na Nevada nchini Marekani huku watabiri wa hali ya hewa wakionya kwamba safari huko Sierra Nevada zitakuwa za tabu kwa siku kadhaa.

Mamlaka karibu na Reno ilisema watu watatu walijeruhiwa katika mrundikano wa magari 20 kwenye eneo la makutano la barabara kuu namba 395 ambapo madereva walielezea hali ya hewa kubadilika na kukosa uwezo wa kuona vyema hapo Jumapili.

Kipande cha maili 70 sawa na kilomita 112 cha barabara kuu eneo la mashariki kwenye barabara kuu namba 80 kilifungwa hadi Jumatatu kutoka eneo la Colfax huko California kupitia eneo la ziwa Tahoe hadi jimbo la Nevada. Idara ya usafiri ya California pia ilifunga barabara nyingine nyingi huku ikionya madereva kuhusu hali ya utelezi kwenye barabara.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG