Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 09:48

Darzeni ya watu huko Ukanda wa Gaza wauawa katika mashambulizi mapya ya Israel


Waandamanaji wakikabiliwa na vikosi vya usalama vya Palestina katika maandamano yaliyofanyika Ramallah wakati Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alipokutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel Ukingo wa Magharibi Jan. i10, 2024.
Waandamanaji wakikabiliwa na vikosi vya usalama vya Palestina katika maandamano yaliyofanyika Ramallah wakati Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alipokutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel Ukingo wa Magharibi Jan. i10, 2024.

Mashambulizi ya Israeli yameua darzeni za watu huko Ukanda wa Gaza katikati ya mashambulizi mapya ya kijeshi huko katikati na kusini mwa Gaza.

Jeshi la Israeli lilisema Jumatano limepiga malengo 150 katika eneo la Maghazi katikati ya Gaza na eneo la Khan Younis upande wa kusini wa eneo finyu la Wapalestina. Iliwaelezea wale waliouawa kuwa ni "magaidi."

Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza ilisema watu 70 waliuawa na 130 kujeruhiwa katika mashambulizi ya usiku kucha. Wizara hiakuweza kutofautisha katika idadi iliyotoa kati ya mauaji ya raia na wapiganaji.

Ghasia zinazoendelea zimekuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa bado yuko katika eneo katika kampeni yake ya kufikia malengo kadhaa, ikiwemo kujaribu kuzuia vita visisambae.

Blinken pia amejaribu kuishinikiza Israel kuepusha vifo vya raia na kufanikisha ufikishaji wa misaada huko Gaza, na amejadili juhudi za kuachiliwa kwa mateka waliobaki wanaoshikiliwa na wanamgambo huko Gaza.

Katika mikutano na viongozi wa kanda hiyo, Blinken alijadili uongozi utakaosimamia Gaza baada ya vita na njia za kuhamasisha amani kati ya Wasraeli na Wapalestina.

Maafisa wa Israeli wamesema mapigano hayo yataendelea kwa miezi kadhaa ijayo wakati jeshi likimaliza udhibiti wa Hamas huko Ukanda wa Gaza, likimaliza tishio la kikundi cha wanamgambo kwa Israel na kuwakomboa mateka 129 ambao wanasaidikiwa bado wanashikiliwa na Hamas.

Hamas iliuwa watu 1,200 katika shambulizi la Oktoba ndani ya Israel na kuwateka watu 240. Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas ilisema mashambulizi ya kujibu uvamizi huo yameuwa zaidi ya Wapalestina 23,300. Eneo kubwa la Gaza limebakia ni vifusi na asilimia 85 ya wakazi wake milioni 2.3 wamekoseshwa makazi.

Umoja wa Mataifa umeonya athari mbaya ya mgogoro huu kwa raia wa Gaza, huku wengi ya watu huko wakiwa wamekimbia makazi yao, na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na afya wakikabiliwa na tatizo la kutoa misaada.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zimetolewa na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG