Misri inashirikiana mpaka wa kilometa 13 na Gaza, ni mpaka pekee uliopo katika pwani ya Palestina ambao haudhibitiwi moja kwa moja na Israel.
Pamoja na Qatar, Misri pia ina jukumu la kuongoza mazungumzo katika kusimamia sitisho jipya la mapigano huko Gaza na kufanikisha makubaliano ya kuachiliwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.
Vyanzo vya Misri vimesema wakati wa mazungumzo hayo Israel iliieleza Misri kuhusu uimarishaji wa njia ya Philadelphi, eneo jembamba lisilo na silaha kwenye mpaka, kama sehemu ya mipango ya Israel kuzuia mashambulizi ya baadaye.
Mgogoro wa sasa umeanza Oktoba 7, wakati Hamas ilipoanya uvamizi ambapo Israel imesema watu 1,200 waliuawa na wengine wapatao 240 kuchukuliwa mateka.
Israel imelipiza kisasi Israel imelipiza kisasi kwa mashambulizi
yaliyoua zaidi ya watu 23,000, kulingana na maafisa wa Gaza, na kuwafanya watu zaidi ya milioni 2.3 kuzikimbia nyumba zao.
Forum