Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema Jumatatu viongozi wa Mashariki ya Kati wamedhamiria kuzuia mgogoro wa Gaza kuenea na kwamba kuna utambuzi mpana juu ya haja ya "kuweka njia ya kisiasa kwa Wapalestina.
Ukingo wa Magharibi na Gaza zinapaswa kuungana kuwa chini ya utawala wa Palestina, Blinken aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Al Ula nchini Saudi Arabia.
Mustakabali wa eneo hilo unahitaji kuwa moja ya muingiliano, sio mgawanyiko na sio migogoro, alisema Blinken, akiongeza ili hilo litokee, tunahitaji kuona kuanzishwa kwa taifa huru la wa-Palestina.
Forum