Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, katika ujumbe wake wa hivi karibuni wa kudhibiti vita vya Gaza, amesema Wapalestina waliokoseshwa makazi lazima waweze kurejea nyumbani mara tu masharti yatakaporuhusu, na Israel imekubali kuruhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa kutathmini hali katika eneo la kaskazini mwa Gaza lililoharibiwa na vita.
“Wakati kampeni ya Israel ikielekea katika awamu ya chini kaskazini mwa Gaza na wakati Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF) vinapopunguza vikosi vyake huko, tumekubaliana leo juu ya mpango wa Umoja wa Mataifa kufanya kazi ya tathmini. Itaamua nini kifanyike ili kuwaruhusu Wapalestina waliokoseshwa makazi kurejea salama katika nyumba zao huko kaskazini”, Blinken aliwaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano wake hapo Jumanne mjini Tel Aviv.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu pia amewataka viongozi wa Israel kuzuia madhara zaidi kwa raia wa Palestina.
Forum