Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:45

COVID-19 : Trump akadiria kuwepo vifo zaidi vya Wamarekani


Rais Donald Trump akishiriki katika mkutano kupitia mtandao wa mawasiliano ya video akihojiwa na kituo cha televisheni cha Fox News, Mei 3, 2020 REUTERS/Joshua Roberts
Rais Donald Trump akishiriki katika mkutano kupitia mtandao wa mawasiliano ya video akihojiwa na kituo cha televisheni cha Fox News, Mei 3, 2020 REUTERS/Joshua Roberts

Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza idadi ya makadirio yake ya vifo vitakavyo tokana na COVID-19, akiahidi kuongeza msaada wa kiuchumi wakati akiwa na matarajio ya kufungua tena shughuli za kawaida nchini.

“Tutapoteza kati ya watu 75, 80 hadi 100,000. Hilo ni jambo baya,“ Trump alisema hayo wakati wa mahojiano katika mkutano kwa njia ya mtandao wa mawasiliano ya video uliorushwa na kituo cha televisheni cha Fox News Jumapili usiku.

Wiki iliyopita Trump alikadiria kuwa vifo kutokana na virusi vya corona vitakuwa kati ya watu 60,000 na 70,000.

Wakati Baraza la Seneti likijitayarisha kukutana Jumatatu, Trump amesema serikali kuu inaweza kuongeza maradufu msaada wa dharura wa hivi sasa wa dola trilioni 3.

Hadi hivi sasa, fedha hizo zimepelekwa kusaidia biashara ndogo kuweza kujiendeleza, kupeleka mahitaji ya hospitali, na kuwapa walipa kodi fedha za matumizi.

“Kuna msaada zaidi unakuja,” Trump amesema.

Kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell amesema baraza litarejea kazini kuendelea kuchukua hatua kukabiliana na COVID-19 na vile vile mambo mengine muhimu.

“Kote katika taifa letu, wafanyakazi wa Marekani katika sekta muhimu wanafuata ushauri wa wataalam na kuchukuwa tahadhari mpya wakati wakihudhuria kazini na kufanya kazi ambazo hazina njia mbadala ambazo nchi inahitaji huduma hizo. Kuanzia Jumatatu, Baraza la Seneti nalo litafanya hivyo,” McConnell amesema katika tamko lake.

Viongozi wa Baraza la Wawakilishi mpaka hivi sasa hawajatangaza mipango ya kukutana mjini Washington, wakati wakitafuta ushauri kutoka kwa madaktari wa bunge juu ya njia salama zaidi za kukutana.

XS
SM
MD
LG