Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:23

China yaapa kulipiza kisasi dhidi ya Taiwan


Spika wa Baraza la Wawakilishi Kevin McCarthy, Mrepublikan, akiwa na Rais wa Taiwan President Tsai Ing-wen wakati walipokutana katika Maktaba ya Urais ya Ronald Reagan huko Simi Valley, California, April 5, 2023.

China imeapa kulipiza kisasi dhidi ya Taiwan baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani na Rais wa kisiwa hicho kukutana, akisema kuwa Marekani iko katika “njia potofu na ya hatari sana.”

Spika Kevin McCarthy alikuwa mwenyeji wa Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen siku ya Jumatano katika hatua ya kuonyesha kuwa Marekani inakiunga mkono kisiwa hicho kinachojitawala, ambacho China inadai ni himaya yake, pamoja na ujumbe wa wabunge zaidi ya darzeni moja wa Marekani kutoka vyama vyote viwili.

Utawala wa Biden unaendelea kusisitiza kuwa hakuna kitu chochote cha uchokozi kuhusu ziara hiyo ya Tsai, ikiwa ni ya hivi karibuni kati ya nusu darzeni za ziara alizofanya Marekani. Na imekuja wakati uhusiano wa Marekani na China umeporomoka sana kwa viwango vya chini kihistoria, huku uungaji mkono wa Marekani kwa Taiwan ukiwa ni moja ya masuala makuu kwa tofauti zilizopo kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu.

Lakini muonekano rasmi wa mkutano huu, na maafisa wa ngazi ya juu baadhi ni maafisa waliochaguliwa katika ujumbe huo kutoka Bunge la Marekani, unaweza kupelekea China kuona kuwa ni uchochezi. Hakuna spika anayejulikana kukutana na rais wa Taiwan katika ardhi ya Marekani tangu Marekani ilivyovunja mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1979.

Ikijibu kuhusu mkutano huo, Beijing ilisema itachukua uamuzi na hatua za mabavu kutetea uhuru wa taifa na heshima ya mipaka yake,” katika taarifa iliyotolewa mapema Alhamisi asubuhi na Wizara ya Mambo ya Nje.

Imeisihi Marekani “iache kufuata mkondo wenye makosa na njia potofu.”

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

XS
SM
MD
LG