Ireland Kaskazini imekuwa bila ya utawala kwa takriban miaka miwili baada ya DUP kujitoa ikipinga kanuni za biashara, ambazo ilisema zilikuwa zikiweka vizuizi na nyingine zote za Uingereza na kuikandamiza nafasi ya Ireland Kaskazini katika hilo.
Kurejea katika serikali kwa chama kikubwa cha kikanda chenye kuunga mkono chama cha Uingereza kinatoa njia ya kutatua mgogoro ambao ulikuwa ni tishio la suluhu ya kisiasa ambayo inaendelea kushikilia makubaliano ya amani ya 1998 ya Ireland Kaskazini, na inamaliza moja ya vipengele vigumu kabisa vya hatua ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya.
“Ninayo furaha kuripoti kuwa mtendaji wa chama hivi sasa ameidhinisha mapendekezo niliyowasilisha kwao,” Jeffrey Donaldson aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mapema Jumanne asubuhi baada ya kuwapa muhtasari wa saa moja wabunge wa DUP na wanachama wake.
“Ikitegemea na ulazima wa kufuata makubaliano kati ya chama cha Democratic Unionist na serikali ya Uingereza kutekelezwa kikamilifu na kwa ukweli kama ilivyokubaliwa… jumla ya hatua hizo kwa jumla zinatoa msingi kwa chama chetu kuwapendekeza wanachama kuingia katika bodi ya utendaji ya Ireland ya Kaskazini,” aliongeza.
Makubaliano yoyote yako hatarini kuigawanya DUP wakati ikiwapa nguvu wapinzani kikiwemo chama kidogo kabisa cha Traditional Unionist Voice, wanaopinga makubaliano yoyote, kabla ya uchaguzi mkuu Uingereza utakaofanyika mwishoni mwa Januari mwaka ujao.
Mapema takriban waandamanaji 50, baadhi yao wakibeba bendera za Union Jack na alama zikisoma “Sitisha Kuisaliti DUP,” walikusanyika nje ya hoteli ambapo Donaldson alikuwa akiwapa muhtasari yaliyojiri kwa wanachama wa chama hicho baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo ya karibu.
Kiongozi wa DUP alisema chama hicho kimefanya maamuzi mazito na matokeo ya kura hiyo yalikuwa “wazi kabisa.”
Donaldson alisema hatua hizo, ambazo zitasimamiwa na sheria mpya za Uingereza, zitaondoa ukaguzi kwa bidhaa ndani ya Uingereza na kubakia Ireland Kaskazini, ikihakikisha hakuna kizuizi dhidi ya biashara za Ireland Kaskazini kuingia katika soko la Uingereza na kulinda nafasi ya kanda hiyo ndani ya Uingereza.
Alisema Uingereza itachapisha maelezo zaidi “muda ujao” na inaweza kuharakisha kuiwezesha DUP kuchukua nafasi yake ya awali katika Bunge la Stormont, Belfast.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum