Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:53

Uingereza imechapisha makubaliano yake ya biashara na EU


Waziri Mkuu Boris Johnson akizungumzia matokeo ya mazungumzo ya Brexit, Dec. 24, 2020
Waziri Mkuu Boris Johnson akizungumzia matokeo ya mazungumzo ya Brexit, Dec. 24, 2020

Maelezo ya Jumamosi yanajumuisha waraka wa biashara wenye kurasa 1,246 ikiwemo makubaliano juu ya nishati ya nyuklia, kubadilishana habari za siri na mifululizo ya maazimio ya pamoja

Uingereza imechapisha maelezo ya makubaliano yake finyu ya biashara na Umoja wa ulaya, siku tano tu kabla ya kutoka katika moja ya umoja mkubwa zaidi wa kibiashara Duniani, katika mabadiliko yake makubwa ulimwenguni, tangu kupotea kwa himaya.

Maelezo hayo ya Jumamosi yanajumuisha waraka wa biashara wenye kurasa 1,246 pamoja na makubaliano juu ya nishati ya nyuklia, kubadilishana Habari za siri na mifululizo ya maazimio ya pamoja.

Rasimu ya mkataba wa biashara na ushirikiano wa EU na Uingereza inamaanisha kuwa kuanzia saa tano usiku kwa saa za huko ifikapo Disemba 31, wakati Uingereza hatimaye inaondoka katika soko moja na umoja wa forodha la Umoja wa ulaya, hakutakuwa na ushuru au mgao juu ya usafirishaji wa bidhaa zinazotoka sehemu yeyote kati ya Uingereza na EU.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson aliutaja mpango huo kama utekelezaji wa mwisho wa matakwa ya watu wa Uingereza ambao walipiga kura asilimia 52 dhidi ya 48 kwa Brexit katika kura ya maoni mwaka 2016 wakati viongozi wa ulaya walisema ni wakati wa kuiacha nyuma Brexit.

XS
SM
MD
LG