Jenerali Honore Traore, Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso alichukua rasmi madaraka ya nchi siku ya Ijuma kufuatia kujiuzulu kwa Rais Compaore baada ya maandamano ya wananchi kupinga juhudi za kubadili katiba ili kuongeza muda wa utawala.
Jeshi lachukua madaraka Burkina Faso

5
Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (kati kati),akizungumza kwenyemkutano na waandishi habari kutangaza kwamba anachukua madaraka ya nchi akiwa katika makao makuu ya jeshi mjini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, Oct. 31, 2014.

6
Waburkinabe wanasherekea tangazo la kuondoka madarakani kwa Rais Blaise Compaore baada ya kukabiliwa na upinzani mkali wa wananchi, Oct. 31, 2014.

7
Wapinzani wa serikali wamekusanyika kwenye Uwanja wa Taifa mjini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, ili kuhakikisha na kusherekea kuondoka madarakani kwa Compaore Oct. 31, 2014.

8
Watu wapora nyumba ya Francois Compaore, kaka yake mdogo rais wa zamani Blaise Compaore, mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Oct. 31, 2014.