Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:37

Bunge la Uganda lavutana juu ya ukomo wa umri wa urais


FILE - Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni delivers a speech during the launch of the National Dialogue committee in Juba, South Sudan, May 22, 2017
FILE - Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni delivers a speech during the launch of the National Dialogue committee in Juba, South Sudan, May 22, 2017

Pendekezo la kuondoa ukomo kwa mgombea urais Uganda lilowasilishwa bungeni limesababisha mvutano mkubwa uliopelekea uvunjifu wa amani ndani ya Bunge

Mbunge anaeiunga mkono serikali ya Uganda aliwasilisha hatua ya kuongeza muda wa rais kugombea nafasi hiyo na kupelekea vurugu ndani ya ukumbi wa Bunge ambapo ililazimu maafisa wa ulinzi kuwaondoa kwa nguvu kutoka katika ukumbi huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP kuondolewa kwa wabunge hao kumekuja baada ya Spika wa Bunge ambaye ni mwanachama wa chama tawala alipowashutumu baadhi ya wabunge kwa kuvuruga utaratibu wa kikao cha Jumanne.

Hili lilitokea wakati wawakilishi walipowasilisha juhudi za kuelezea muswada wa kuondoa umri wa rais wa miaka 75 kutoka kwenye katiba ya Uganda na kufuta kipengele cha umri.

Picha kutoka kikao cha bunge zilionyesha baadhi ya wabunge wa upinzani wakivutwa na kutolewa nje na wengine kuburuzwa na maafisa usalama ambao hawakuvaa sare za polisi.

Kiongozi wa upinzani baada ya kulalamika kwamba kikosi maalumu kilitumiwa kuwatoa nje wabunge wenzake baadae aliongoza timu yake kutoka nje.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni

Rais Yoweri Museveni ambaye ana umri wa miaka 73 na ametawala Uganda tangu alipochukua madaraka kwa nguvu mwaka 1986 hastahili kuwania tena kiti hicho mwaka 2021 kama kipengele kinachozungumzia umri bado kitakuwepo ndani ya katiba ya Uganda. Rasimu ya mswaada lazima itangazwe katika gazeti la serikali kabla kujadiliwa katika bunge la taifa.

Hatua ya kuondoa kiwango cha umri imeonekana kama juhudi za Museveni kuongeza utawala wake. Rais Museveni amelikwepa swali iwapo ana nia ya kuwepo zaidi madarakani akisema hivi karibuni kwamba suala hilo sio muhimu. Lakini wakosoaji wanasema pembeni na mazungumzo hayo anaongoza hatua hiyo kwa wabunge kuondoa kipengele cha mwisho ili kuongeza muda wake wa urais ikiwezekana aongoze taifa hilo hadi kifo kitakapomkuta.

Kipengele cha rais kuhudumu kiliondolewa kutoka katika katiba ya Uganda ya mwaka 2005. Chama tawala nchini Uganda kinafurahia wingi wa wawakilishi wake katika bunge na mswaada unatarajiwa kupitishwa.

XS
SM
MD
LG