Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:47

Biden atarajiwa 'kuhamasisha mtizamo wa pamoja kwa Amerika Kaskazini'

Rais Joe Biden awasili Mexico.
Rais Joe Biden awasili Mexico.

Jean-Pierre alisema Biden atatoa matangazo kadhaa kuhusu kupanua ushirikiano katika kupambana na usafirishaji haramu wa silaha, dawa ya kulevya na binadamu, hali kadhalika kuhughulikia changamoto za mazingira na hatua “za pamoja kuzungumzia  uhamiaji usiokuwa wa kawaida katika kanda hiyo.”

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador atakuwa mwenyeji wa Rais wa Marekani Joe Biden kwa mazungumzo Jumatatu huko Mexico City kabla ya mkutano wa viongozi wa kanda ambao utamjumuisha Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Uhamiaji, mabadiliko ya hali ya hewa, biashara na uzalishaji ni miongoni mwa mada kuu katika ajenda hiyo.

Msemaji wa White House Karine Jean-Pierre alisema kuwa katika ziara yake Mexico ambayo ni ya kwanza tangu kuwa rais, Biden anataraji “kuhamasisha mtizamo wa pamoja kwa Amerika Kaskazini.”

Jean-Pierre alisema Biden atatoa matangazo kadhaa kuhusu kupanua ushirikiano katika kupambana na usafirishaji haramu wa silaha, dawa ya kulevya na binadamu, hali kadhalika kuhughulikia changamoto za mazingira na hatua “za pamoja kuzungumzia uhamiaji usiokuwa wa kawaida katika kanda hiyo.”

Biden asimama katika daraja la mlango wa bandari ya Marekani na azungumza na maafisa wa forodha na ulinzi wa mpakani na kumuonyesha vifaa vinavyotumika kukagua magari katika mpaka wa Marekani na Mexico, mji wa El Paso, Texas, Jan. 8, 2023.

Kabla ya mkutano huo wa Jumanne, Biden, Trudeau na Lopez Obrador watajumuika pamoja na wake zao katika chakula cha usiku.

Biden aliwasili jioni Jumapili huko Mexico baada ya kuutembelea mji wa Texas wa El Paso kujionea wimbi la maelfu ya wahamiaji wasiokuwa na makaratasi wakivuka mpaka wa Mexico.

Wakati wa ziara yake ya takriban saa nne katika mji wa mpakani, Biden alisimama katika daraja la mlango wa bandari ya Marekani ambako alikutana na maafisa wa forodha na ulinzi wa mpakani na kuangalia wakati wakimuonyesha namna wanavyokagua magari kwenye mpaka kutafuta dawa za kulevya, fedha na bidhaa feki.

Biden pia alitembea katika eneo la ukuta wa mpaka wa Marekani na Mexico unaoutenganisha mji wa Texas kutoka Ciudad Juarez. Maafisa wawili wa Doria ya Mpakani walitembea na rais.

Pia alitembelea kituo cha kuwasaidia wahamiaji katika Kaunti ya El Paso ambako alikutana na maafisa wa eneo na viongozi wa jamii.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na shirika la habari la AP.

XS
SM
MD
LG