Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 14:40

Hali mbaya ya hewa Marekani yasababisha vifo na uharibifu wa mali


Hali mbaya ya hewa marekani imesababisha takribani ndege 6,400 kuahirisha safari zake
Hali mbaya ya hewa marekani imesababisha takribani ndege 6,400 kuahirisha safari zake

Mamia ya safari za ndege zimefutwa na kunatarajiwa kutokea kimbunga kibaya sana wakati kukiwa na shinikizo baya la kushuka kwa viwango vya hali ya hewa  karibu na Great Lakes na kupelekea upepo mkali na theluji.

Mamilioni ya watu walijifungia majumbani Jumapili ili kuepuka dhoruba ya majira ya baridi kali iliyouwa watu 34 kote nchini Marekani na inatarajiwa kusababisha vifo zaidi baada ya wakaazi wengi kukwama ndani ya nyumba zao kutokana na theluji.

Hali hiyo imesababisha umeme kukatika katika maelfu ya nyumba na biashara.

Dhoruba ambayo haikutarajiwa imekuwa kubwa kuanzia eneo la Great Lakes karibu na Canada hadi Rio Grande kwenye mpaka na Mexico. Karibu asilimia 60 ya watu nchini Marekani wamekabiliwa na tufani ya hali hiyo iliyosababisha maonyo ya hali ya hewa katika kipindi hiki cha baridi kali. Viwango vya hali ya hewa vimeshuka sana kuliko kawaida kutoka mashariki mwa milima ya Rocky hadi Appalachians idara ya kitaifa ya hali ya hewa imesema.

Matatizo kwa wasafiri kutokana na hali ya hewa huenda yakaendelea huku mamia ya safari za ndege zikifutwa na kunatarajiwa kutokea kimbunga kibaya sana wakati kukiwa na shinikizo baya la kushuka kwa viwango vya hali ya hewa karibu na Great Lakes na kupelekea upepo mkali na theluji.

Kulingana na tovuti inayofuatilia safari za ndege ya Flightware. Baadhi ya safari za ndege takriban 1,707 za ndani na za kimataifa zilifutwa Jumapili mchana .

Gavana wa New York Kathy Hochul amesema karibu kila gari la zimamoto kwenye mji huo lilikwama Jumamosi na aliwasihi watu kuheshimu marufuku iliyotolewa ya kutoendesha gari katika eneo hilo.

“Bado tuko kwenye hali hii ya hatari sana na inayotishia maisha. Kwasababu tu watu wanaweza kuona mwanga kidogo leo, dhoruba hizo, upepo mkali , ukubwa wa hali hiyo, itarudi tena usiku wa leo. kwa hiyo ujumbe wa kwanza nataka kusisitza kwa watu nilioko nao hapa leo, mnatakiwa kutokuwepo barabarani, tumekuwa tukiwaomba, tumekuwa tukiwaasa.”

Watabiri wa hali ya hewa wameonya kutakuwa na theluji nyingine itakayonyesha na ina uwezekano wa futi moja hadi mbili katika baadhi ya maeneo mapema Jumatatu ikiambata na upepo wa kasi ya maili 40 kwa saa.

XS
SM
MD
LG