Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 11:11

Mexico: Watu wenye silaha washambulia gereza na kuua watu 14


Ramani ya Mexico
Ramani ya Mexico

Watu wenye silaha Jumapili walilishambulia gereza katika mji wa kaskazini mwa Mexico wa Ciudad Juarez, na kuua watu 14 na kuruhusu wafungwa 24 kutoroka, ofisi ya waendesha mashtaka wa jimbo la Chihuahua imesema.

Idadi isiyojulikana ya watu wenye silaha waliokuwa ndani ya magari ya kivita walihusika katika shambulio hilo, miongoni mwa waliouawa ni walinzi wa gereza na maafisa wa usalama kumi, imesema taarifa ya ofisi ya waendesha mashtaka.

Shambulio hilo lilitokea majira ya saa moja asubuhi kwa saa za huko na kuzua mapigano kati ya wafungwa ndani ya gereza hilo waendesha mashtaka wamesema.

Muda mfupi kabla ya shambulio, watu wenye silaha waliwafyatulia risasi polisi wa manispaa kwenye barabara kuu ilio karibu na gereza hilo, na kulifanyika msako wa gari ambao ulimalizika kwa kulikamata gari moja na wanaume wanne, taarifa iliongeza.

Ofisi hiyo imesema, baadaye washambuliaji waliokua ndani ya gari aina ya Hummer walilifyatulia risasi kundi jingine la maafisa nje ya gereza.

Waendesha mashtaka wamesema mapigano ndani ya gereza, ambapo wafungwa kutoka vikundi tofauti vya uhalifu na magenge yanayofanya biashara ya dawa za kulevya wamewekwa katika vyumba tofauti vya gereza, pia watu 13 walijeruhiwa katika mapigano hayo.

XS
SM
MD
LG