Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:20

Biden kukutana na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau wakati wa ziara yake nchini Mexico


Rais wa Marekani Joe Biden akitembea na maafisa wa mpakani karibu na ukuta unaogawanyisha Marekani na Mexico. Jumapili Januari 8,2023
Rais wa Marekani Joe Biden akitembea na maafisa wa mpakani karibu na ukuta unaogawanyisha Marekani na Mexico. Jumapili Januari 8,2023

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Abrador  Jumatatu ni mwenyeji wa rais wa Marekani Joe Biden huko  Mexico City kabla ya kikao cha kieneo kitakachoshirikisha waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Uhamiaji, mabadililo ya hali ya hewa, biashara na viwanda ni baadhi ya masuala yanayotarajiwa kutawala ajenda ya kikao hicho. Biden aliwasili Mexico Jumapili jioni baada ya kuutembelea mji wa mpakani wa El Paso katika jimbo la Texas, ili kujionea mwenyewe maelfu ya wahamiaji wasio na stakabadhi, wanaojaribu kuingia Marekani wakitokea Mexico.

Biden aliyechukua takriban saa nne kwenye mpaka huo alifuatana na maafisa wa mpakani huku akijionea namna wanavyokagua magari wakitafuta dawa za kulevya, usafirishaji haramu wa fedha, pamoja na bidhaa nyingine kinyume cha sheria.

Biden pia aliandamana na maafisa hao kwenye uzio unaotenganisha Marekani na Mexico. Pia alitembelea kituo cha uhamiaji cha El Paso ambako alikutana na maafisa wa uhamaji pamoja na viongozi wa kijamii.

Baada ya kuutembelea mpaka huo, Biden aliweka ujumbe kwenye Twitter akiesema kwamba inawezekana kuulinda mpaka wa Marekani na Mexico na kuufanya mpaka huo kuwa salama kwa wahamiaji.

XS
SM
MD
LG