Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 21:13

Bashir yupo tayari kuandaa mazungumzo ya Sudan Kusini


Rais wa Sudan, Omar al-Bashir
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Sudan ilitangaza kwamba Rais Omar Al- Bashir wa nchi hiyo yuko tayari kuandaa mazungumzo ya amani kati ya mahasimu wawili wakuu wa Sudan Kusini, Rais Salva kiir na Riek Machar.

Maafisa wa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Khartoum walisema kwamba pendekezo la Rais Bashir liliwasilishwa kwa Rais Kiir na ujumbe wa Sudan uliotembelea Juba siku ya Jumanne na umewasilishwa siku chache tu baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio linalozipatia pande zinazogombana Sudan Kusini mwezi mmoja kuweza kufikia makubaliano ya amani au kukabiliwa na vikwazo vikali zaidi.

Riek Machar (L) na Rais Salva Kiir, wakiwa Juba, April 29, 2016.
Riek Machar (L) na Rais Salva Kiir, wakiwa Juba, April 29, 2016.

​Ujumbe wa Sudan uliongozwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa sudan Al- Dierdiry al-dhikheri . Rais Salva kiir wa Sudan Kusini anaripotiwa kupokea juhudi hizo na kuthibitisha kwamba serikali yake iko tayari kushiriki kwenye mazungumzoi hayo. Siku ya kufanyika mazungumzo hayo ya amani bado haijatajwa.

XS
SM
MD
LG