Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 03:14

Baraza la Wawakilishi kutoa ripoti ya uvamizi wa Bunge la Marekani kesho


U.S. Capitol Congress

Kamati ya Baraza la Wawakilishi la Marekani inayochunguza uvamizi uliotokea kwenye jengo la bunge Januari 6 inatarajiwa kutoa ripoti yake kesho Alhamisi.

Ripoti hiyo itatoa fursa ya kuanzishwa kwa mjadala kuhusu rekodi ya kihistoria kuhusiana na sababu na athari za shambulizi hilo lililofanywa na wamarekani dhidi ya serikali.

Kamati hiyo inatarajiwa kutoa utangulizi wa maelezo kuhusu uchunguzi wake wa miezi 11 Alhamisi usiku.

Zaidi ya watu 1000 wamehojiwa na kamati hiyo, na maelezo machache sana kuhusu uchunguzi huo yametolewa kwa umma, hasa kupitia mahakamani, wakati kesi kuhusu washukiwa zinaposikilizwa.

Watu 800 wamefunguliwa mashtaka kuhusiana na shambulizi dhidi ya bunge lililotokea Januari 6 na watu kadhaa wanaendelea kukamatwa kila wiki kuhusiana na tukio hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG