Kikao hicho kitahusu hatua ya Russia kupeleka wanajeshi wake karibu na Ukraine, na wadau wote muhimu wanatarajiwa kujitokeza hadharani dhidi ya uwezekano wa uvamizi wa Russia.
Mkutano wa Jumatatu huko New York umekuja siku chache baada ya maonyo makali kutoka nchi za Magharibi kuwa Moscow inaweza kuivamia Ukraine mwezi Januari.
Kukataa kwa Moscow na maombi kutoka kwa rais wa Ukraine kusema hakuna haja ya taharuki zisizo za lazima yameshindwa kupunguza wasiwasi unaoongezeka.
Washirika wa Magharibi wa Kyiv ikiwemo Marekani na Umoja wa Ulaya wamerudia kutishia kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia kama itaingiza wanajeshi wake Ukraine.
Hata hivyo Moscow imeitaka NATO kupunguza shughuli zake mashariki mwa Ulaya na kamwe kutoiruhusu Ukraine kuwa mwanachama wake.