Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 18:26

Blinken atembelea Ukraine huku ukiwepo wasiwasi wa Russia kuishambulia


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameitembelea Ukraine wakati utawala wa Rais Joe Biden umetangaza msaada wa ziada wa dola milioni 200 kwa ajili ya Ukraine kujiimarisha kijeshi huku kukiwepo wasiwasi wa Russia kuishambulia nchi hiyo.

Blinken amewaambia wafanyakazi katika ubalozi wa Marekani mjini Kyiv kwamba Rais wa Russia Vladmir Putin anapanga kuongeza idadi wanajeshi 100,000 zaidi kwenye mpaka wa Ukraine.

Waziri Blinken amefafanua kuwa: "Tumekuwa tukijihusisha na hali ya Ukraine katika miezi kadhaa iliyopita kutokana na Russia kuendelea kuongeza wanajeshi wake karibu na mpaka na Ukraine. Hakuna uchokozi wala sababu lakini tuna nguvu za kutosha. Tunajua kwamba s kuna mipango y akuongeza idadi ya wanajeshi hao kwatika muda wa siku chache. Na hilo linatoa nguvu kwa rais Putin kwa muda mfupi kuishambulia Ukraine.

Blinken amesema uchokozi wa Russia kwa Ukraine unavunja kanuni za msingi kama mataifa hayawezi kutumia ushawishi wao kujaribu kuvuruga haki ya majirani zake.

Blinken ameongezea kwamba utawala wa Biden umejaribu kuweka wazi kwamba kuna njia mbili kwa Russia; njia ya mazungumzo ili kusuluhisha tofauti zozote zilizopo kwa njia ya amani na diplomasia, ambayo ndio tunayoipendelea. Lakini pia kuna njia ambayo huenda Russia ikaamua, kufanya mashambulizi, ambayo ina athari zake.

XS
SM
MD
LG