Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:21

Waziri wa mambo ya nje wa Canada kutembelea Kyiv


Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Melanie Joly alipowasili kwenye kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo wa G-7 na nchi waalikwa mataifa ya ASEAN.huko Liverpool Uingereza.
N nations in Liverpool, England, Dec. 12, 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Melanie Joly alipowasili kwenye kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo wa G-7 na nchi waalikwa mataifa ya ASEAN.huko Liverpool Uingereza. N nations in Liverpool, England, Dec. 12, 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Melanie Joly atatembelea Kyiv wiki ijayo ili kuthibitisha kuunga mkono mamlaka ya Ukraine na kuimarisha juhudi za kuzuia vitendo vya uchokozi vinavyofanywa na Russia, Ottawa imesema Jumamosi.

Moscow imeweka zaidi ya wanajeshi 100,000 karibu na mpaka na Ukraine na Marekani ilisema siku ya Ijumaa kuwa inahofia Russia ilikuwa inaandaa kisingizio cha kuivamia iwapo diplomasia itashindwa kufikia malengo yake.

Canada, yenye wakazi wengi na wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa wa asili ya Ukraine, imechukua msimamo mkali na Moscow tangu kujiingiza huko Crimea mwaka 2014.

Kupelekwa kwa wanajeshi na vifaa vya Russia ndani na kuzunguka Ukraine kunahatarisha usalama katika eneo lote. Hatua hizi za kichokozi lazima zizuiwe, Joly alisema katika taarifa yake.

XS
SM
MD
LG