Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:16

Blinken aidhinisha nchi za Baltic kupeleka silaha za Marekani nchini Ukraine


U.S. Secretary of State Blinken speaks to the media in Geneva
U.S. Secretary of State Blinken speaks to the media in Geneva

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Jumamosi ametoa idhini kwa nchi za Baltic za Estonia, Latvia na Lithuania kupeleka makombora yaliyotengenezwa Marekani ya kupambana dhidi ya vifaru na ndege za kivita kwenda Ukraine, hatua ilikuja wakati Ukraine ikiwa katikati ya mivutano inayoongezeka na jirani yake Russia.

“Nimeharakisha na kuidhinisha, na tumepitisha kikamilifu uhamishaji wa vifaa vya ulinzi vilivyopo kwa washirika wa NATO Estonia Latvia Lithuania watawapa Ukraine ili kuimarisha uwezo wake wa kujihami dhidi ya vitendo vya uchokozi usiokuwa nauchochezi na visivyo vya uwajibikaji vinavyofanywa na Russia,” Blinken alisema katika ujumbe wa Twitter.

Blinken pia amezishukuru zilizokuwa jamhuri za Umoja wa Soviet na wanachama wa NATO, “kwa msaada wao wa muda mrefu kwa Ukraine.”

Tangazo la Blinken la kuidhinisha kusafirishwa kwa silaha hizo limekuja siku moja baada ya Marekani na Russia kuonekana wamepiga hatua ndogo huku hali ya hatari ya mivutano ikiongezeka juu ya Ukraine, kila upande ukiondoka katika mazungumzo ya ngazi ya juu ya Ijumaa ukiahidi kuendelea kufanya kuzungumza.

Rais wa Marekani Joe Biden aliilenga Ukraine Jumamosi. Katika taarifa White House ilisema, “Rais Biden alikutana na timu yake ya usalama wa taifa binafasi na kupitia njia ya mtandao akiwa Camp David kujadili kuendelea kwa vitendo vya uchokozi vya Russia dhidi ya Ukraine.

Rais Biden alipewa muhtasari juu ya hali ya operesheni za kijeshi zinazoendelea kufanywa na Russia katika mipaka ya Ukraine na “kujadili juhudi zetu zinazoendelea kupunguza hali hiyo kwa njia ya kidiplomasia na hatua zetu mbalimbali kuepusha vita zinazoratibiwa kwa karibu na washirika wetu na wadau, ikiwemo ufikishaji wa misaada wa ulinzi kwa Ukraine.

Kwa mara nyingine Rais Biden amethibitisha kuwa iwapo Russia itaivamia Ukraine, Marekani itajibu kwa haraka na kuchukua hatua kali dhidi ya Russia ikishirikiana na washirika wetu na wadau.”

Mashirika ya habari ya CNN na Fox News yamekuwa yakiripoti Jumamosi kuwa Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv uliitaka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuidhinisha wafanyakazi wasiokuwa muhimu na familia zao kuondoka nchini humo.

Chanzo kilicho karibu na serikali ya Ukraine kimeiambia VOA kuwa walikuwa wamesikia kutoka kwa vyanzo vyao vya Marekani kuwa kuondolewa kwa familia na wafanyakazi wasiokuwa muhimu kunaendelea kufanyiwa tathmini.

Kulingana na chanzo hicho, mpango wa kuondolewa kwa familia na wafanyakazi hao umefikishwa na Marekani kwa serikali ya Ukraine Ijumaa.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo mashirika ya habari ya AFP, AP, Reuters.

XS
SM
MD
LG