Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:12

Baraza la Senati lampitisha Kavanaugh kuwa Jaji Mahakama ya Juu


Wanaharakati nchini Marekani wakipinga uteuzi wa Jaji Brett Kavanaugh kuthibitishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Octoba 6, 2018.
Wanaharakati nchini Marekani wakipinga uteuzi wa Jaji Brett Kavanaugh kuthibitishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Octoba 6, 2018.

Baraza la Seneti limepiga kura Jumamosi kupitisha uteuzi wa Brett Kavanaugh kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu nchini Marekani.

Hatua hii imefikiwa baada ya wiki kadhaa za malumbano juu ya madai ya kashfa ya ngono na ukosoaji wa tabia na mwenendo wake.

Kavanaugh alipitishwa kushika nafasi hiyo kwa hisabu ya kura 50-54. Seneta Mrepublikan Steve Daines wa Montana alikuwa ameshindwa kuwepo kupiga kura kwa sababu alikuwa anahudhuria ndoa ya mtoto wake.

Hilo lilifanya Seneta Mrepublikan Lisa Murkowski wa Alaska kupiga kura ya “nipo” katika utaratibu unaoitwa “kushirikiana” kati ya maseneta.

Murkowski alikuwa amepinga kupitishwa Kavanaugh katika wadhifa wa mahakama ya juu, lakini aliondoa kura yake ya “hapana” ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kushirikiana, ili kwamba Daines asilazimike kuwa katika chumba cha seneti.

Wakati Maseneta wanapiga kura, waandamanaji wanaopinga uteuzi huo wakiwa ndani ya eneo la Seneti walipiga makelele, “Siungi mkono hilo!” na ni “fedheha!”

Makamu wa Rais Mike Pence, ambaye alikuwa anasimamia kikao hicho, alirejea mara kadhaa kutaka kuwepo na utulivu.

Baada ya kupigwa kura Rais Donald Trump alituma ujumbe wa Tweet : Nalipongeza Baraza la Seneti kwa kumpitisha mteule wetu Bora, Jaji Brett Kavanaugh, kuingia katika Mahakama ya Juu ya Marekani. Baadae leo, nitasaini waraka wa uteuzi wake, na ataapishwa rasmi. “Ni furaha iliyoje!”

Wachambuzi wanasema kuwa kuingia kwa Kavanaugh kutawapa majaji Maconservative kuwa na kura tano za wingi dhidi ya nne katika mahakama hii. Uteuzi huo wa maisha unamaanisha kuwa Kavanaugh, 53, anaweza kutumikia wadhifa huo kwa miongo mingi.

XS
SM
MD
LG