Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:19

Kura ya kumuidhinisha Kavanaugh inaendelea Marekani


Brett Kavanaugh,
Brett Kavanaugh,

Maandamano yanafanyika kote Marekani na nje ya jengo la bunge mjini Washington DC kupinga utaratibu wa kuendelea kumuidhinisha Brett Kavaugh.

Baraza la seneti la Marekani linatarajiwa Jumamosi kuidhinisha uteuzi wa Brett Kavanaugh kuhudumu mahakama ya juu Marekani kufuatia wiki kadhaa za utata kutokana na shutuma za visa vya ngono na mashambulizi mengine yanayohusu tabia yake.

Nafasi ya Kavanaugh kuhudumu kwenye mahakama ya juu Marekani iliongezeka Ijumaa wakati maseneta wawili muhimu, m-Republican Susan Collins na m-Democrat Joe Manchin waliposema watampigia kura ya ndio katika uidhinishwaji wake. Katika hotuba yake kwa seneti, Collins alielezea mapungufu ya ushahidi kwa madai yaliyotolewa dhidi ya Kavanaugh na aliongeza kwamba uamuzi wake usieleweke kama unakataa malalamiko muhimu kuhusu shambulizi la ngono.

Wakati huo huo, Manchin aliandika katika Twitter dakika kadhaa baadae atapiga kura ya ndio kulingana na taarifa aliyoipata ikiwemo repoti iliyokamilika ya karibuni kutoka FBI.

XS
SM
MD
LG