Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 08:02

Armenia yatangaza utawala wa dharura baada ya mapigano kuzuka na Azerbaijan


Vifaru vya Azerbaijani na wanajeshi wake wakati wa shambulizi la mkoa uliojitenga wa Nagorno-Karabakh

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan ametangaza utawala wa kijeshi na kuweka hali ya juu ya tahadhari baada ya mapambano na Azerbaijan katika jimbo linalogombaniwa la Nagorno Karabah. 

Katika ukurasa wake wa Facebook, Pashinyan ameandika, “Kuwa tayari kulinda nchi yetu tukufu.”

FILE - Waziri Mkuu Nikol Pashinyan
FILE - Waziri Mkuu Nikol Pashinyan

Armeni inaituhumu nchi jirani ya Azerbaijan kwa kushambulia makazi ya raia katika jimbo hilo linalogombaniwa.

Wizara ya ulinzi imetoa taarifa ikieleza kwamba jibu lao litakuwa la nguvu sana na uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Azerbaijan wanawajibika kikamilifu na hali hii mpya.

Wizara hiyo imeongeza kusema kwamba wanajeshi wake walitungua helikopta ya jeshi la Azerbaijan na ndege tatu bila ya rubani zilizokuwa zina shambulia jimbo hilo linalotaka kujitenga.

Mashambulio hayo ambayo ndio mabaya tangu 2016 yanazusha hofu ya kuzuka vita vipya kati ya maadui wa muda mrefu, Azerbaijan na Armeni, ambao wamekuwa kwa miongo kadhaa katika hali ya uhasama kwa ajili ya ardhi wanayogombania ya Nagorny Karabakh iliyoko upande wa Azerbaijan, lakini yenye wakazi wake wengi wa Armenia wanaotaka kujitenga.

Viongozi wa Rashia, Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Ulaya, kwa haraka wametoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja, huku Papa Francis akiombea amani kupatikana wakati wa misa yake Jumapili.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Armenia Artsrun Hovhannisyan amesema kumekuwepo na mapigano makali yaliyoendelea hadi mchana wa Jumapili kwenye mpaka wa Karabakh.

Wakazi wa Kiaremania wanaotaka kujitenga kutoka jimbo la Nagorny Karabakh walichukuwa mamlaka ya jimbo kutoka uongozi wa Baku mnamo vita vya miaka 1990 vilivyosababisha vifo vya karibu watu 30,000.

Mazungumzo ya kutanzua moja wapo ya ugomvi mbaya tangu kusambaratika kwa Urusi 1991 kwa sehemu kubwa yamekwama tangu kufikiwa makubaliano ya 1994.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG