Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:58

Mshukiwa ampiga risasi na kumuua afisa wa polisi wakati yuko chini ya ulinzi


Polisi akilinda kituo cha Croydon ambacho mshukiwa alimpiga risasi na kumuua afisa wa polisi akiwa chini ya ulinzi Kusini mea London, Uingereza Sept. 25, 2020.
Polisi akilinda kituo cha Croydon ambacho mshukiwa alimpiga risasi na kumuua afisa wa polisi akiwa chini ya ulinzi Kusini mea London, Uingereza Sept. 25, 2020.

Afisa polisi London amepigwa risasi na kuuawa mapema Ijumaa ndani ya kituo cha polisi wakati wakimshikilia mshukiwa, maafisa wamesema.

Katika taarifa, Polisi wa Metropolitan London wamesema tukio hilo limetokea saa nane na robo alfajiri kwa saa za London katika Kituo cha Mahabusu cha Croydon upande wa kusini wa jiji hilo.

Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limeripoti kuwa mshukiwa mwenye umri wa miaka 23 alikuwa anashikiliwa, alichomoa silaha na kumpiga afisa huyo, na kujipiga mwenye risasi. Polisi wanasema hakuna silaha za maafisa wa polisi zilizopigwa.

Polisi wanasema mshukiwa huyo anatibiwa katika hospitali mjini London, ambapo yuko katika hali mbaya. Afisa huyo hajatambuliwa wakati polisi walipokuwa wakiijulisha familia yake.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, kupitia akaunti yake ya Twitter, alitoa rambirambi kwa familia ya afisa huyo na wafanyakazi wenzake kama alivyofanya Meya wa London Sadiq Khan.

Uingereza inasheria kali za umiliki wa silaha, na ni mara chache kwa maafisa wa polisi kupigwa risasi na kuuawa.

BBC inaripoti afisa wa Croydon ni wa 17 katika jeshi la polisi la London kuuawa kwa silaha ya moto tangu Vita ya Pili ya Dunia.

Shirika hilo la utangazaji linaripoti tangu mwanzoni mwa karne ya 20, ni maafisa polisi 73 tu waliopigwa risasi na kuuawa na wahalifu nchini Uingereza, bila ya kujumuisha vifo huko Ireland ya Kaskazini. Vifo vingi – zaidi ya 50 – vimetokea tangu mwaka 1945.

XS
SM
MD
LG