Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 13:54

Mike Pence akubali kuwa mgombea mwenza wa Rais Trump


US Vice President Mike Pence speaks during the third night of the Republican National Convention at Fort McHenry National Monument in Baltimore, Maryland, August 26, 2020. (Photo by SAUL LOEB / AFP)

Makamu rais, Mike Pence alikuwa msemaji mkuu katika siku ya tatu ya mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican, akiongea kutoka Fort McHenry, Baltimore kukubali uteuzi wa chama chake kuwa mgombea mwenza wa Rais Donald Trump katika uchaguzi wa mwezi Novemba 2020.

Katika matamshi yake, Pence amesema watu wako katika hali ya kukumbwa na kimbunga Laura na hivyo kuwataka waheshimu maonyo kuhusu nguvu ya dhoruba hiyo na kuahidi kuwa utawala wa Trump utawasaidia.

Pence anasema : "Kabla ya kwenda mbali, naomba mniruhusu nisema neno moja kwa familia na jamii ambazo ziko katika eneo ambalo kimbunga Laurant kitapita. Utawala wetu unafanya kazi kwa karibu sana na mamlaka katika majimbo ambayo yatapata athari za kimbunga. FEMA imehamasisha kupata rasilimali na vifaa kwa wale ambao wataathirika. Hii dhoruba ni ya kweli. Tunawasihi wale wote walio katika maeneo yaliyoathiriwa kuheshimu mamlaka ya majimbo na miji. M kae salama, ni vyema mfahamu kamba tutakuwa na nyinyi kuwasaidia katika kila hatua, kuwaokoa, kujibu na kurejea katika hali ya kawaida kwa siku na wiki zitakazofuata. Hicho ndicho wamarekani wanachofanya."

Pence kwa unyenyekevu mkubwa alikubali uteuzi wa Republican kuhudumu kwa mara ya pili kama makamu rais, akisema, "katika nyakati hizi zenye changamoto nyingi, nchi yetu inahitaji rais ambaye anaamini kuhusu Marekani."

Makamu wa Rais Mike Pence na mkewe Karen Pence wakiwasili kwenye mkutano wa chama chake kutoa hotuba ya kukubali kuwa mgombea mwenza wa Rais Donald Trump, Fort McHenry in Baltimore, Maryland, U.S.
Makamu wa Rais Mike Pence na mkewe Karen Pence wakiwasili kwenye mkutano wa chama chake kutoa hotuba ya kukubali kuwa mgombea mwenza wa Rais Donald Trump, Fort McHenry in Baltimore, Maryland, U.S.

"Miaka minne iliyopita, nilijibu wito wa kunitaka nijiunge katika jukumu hili kwasababu nilifahamu kwamba Donald Trump uongozi wake na mtizamo wake kwa Marekani ni mkubwa sana. Katika muda wa miaka minne iliyopita, nimemuangalia rais huyu akivumilia mashambulizi yasiyokwisha na kusimama kila siku kupambana kutimiza ahadi alizotoa kwa watu wa Marekani. Kwahiyo, kwa heshima kubwa na imani ya Rais Donald Trump kwangu mimi, uungaji mkono wa chama changu cha Republican, na uwezo wa mwenyenzi mungu, kwa unyenyekevu mkubwa nakubali uteuzi wenu wa kunitaka niwanie na kuhudumu tena kama makamu rais wa Marekani," alieleza Pence.

Madison Cawthorn, Mrepublican mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mgombea ubunge kutoka North Carolina, alizungumza katika mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican jana usiku. Carthworth aliwataka waliberali kusikiliza mawazo ya watu wengine na kwa waconservative kufafanua kile ambacho wanakiamini.

Cawthorn pia alimzungumzia kiongozi wa kutetea haki za kiraia Dr. Martin Luther King Jr. (MLK) ambaye alizungumza kuhusu ndoto yake ya watu kuangaliwa kulingana na tabia zao, na siyo rangi ya ngozi yao. Amesema mamilioni ya watu ambao wanajaribu kuja Marekani wanakubaliana na ndoto hii.

Madison Cawthorn alisema : "Kuwa mkali kwa uhuru. Kuwa mkali kwa ukombozi, na kuwa mkali kwa jamhuri ambayo mimi nimesimama. Taifa moja chini ya mwenyezi mungu kwa uhuru na haki kwa wote. Ahsanteni sana. Mungu aibariki Marekani."

Rais Donald Trumop anapanga kukubali rasmi uteuzi kuwania awamu ya pili ya uongozi hivi leo Alhamisi, lakini shamra shamra za mkutano mkuu ni kabla ya yeye kupanda jukwaani.

Hans Noel, profesa wa masuala ya siasa za vyama na itikadi katika chuo kikuu cha Georgetown, anasema tarajia Trump kuwa na matamshi ya zaida, badala ya kusoma kile kilichoandikwa mapema katika hotuba yake, ikiwa ni juhudi ya kuwavutia wapiga kura ambao bado hawajaamua wamchague nani.

Profesa Noel alísema :"Tunataka kuwafikia wapiga wetu . ambao kiasili wanakipigia kura chama cha Republican, kuwafikia wapiga kura weusi , wapia kura walatino. Na hivyo tutawaonyesha kwamba tuna watu wawili ambao kama hao ambao wanatupigia sisi kura. Kwahiyo huenda mkawa katika hali nzuri. Na hiyo huo ni sehemu moja ya mkakati."

Pence alihutubia kutoka Fort McHenry, ambako Wamarekani waliitetea Bandari ya Baltimore kutoka kwa Uingereza wakati wa vita vya mwaka 1812 na kumtia hamasa Francis Scott Key kuandika “The Star Spangled Banner.”

Rais, Mke wake Melania, Pence na mkewe Pence walijichanganya katika mkunsanyiko uliokuwepo hapo baada ya Pence kumaliza hotuba yake.

Rais Trump na mkewe Melania wakiwasili katika mkutano mkuu wa Republikan kuzikiliza hotuba ya Makamu wa Rais Mike Pence.
Rais Trump na mkewe Melania wakiwasili katika mkutano mkuu wa Republikan kuzikiliza hotuba ya Makamu wa Rais Mike Pence.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG