Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 06:46

VIJIMAMBO: Mtu atembeaye na kondoo kila pahali


Mtu akimvuta kondoo

Safari yetu ya Vijimambo wiki hii inaanzia mjini Mombasa, pwani ya Kenya. Bwana mmoja ambaye kwa miezi kadhaa sasa amekuwa akitembea kila aendapo akiandamana na kondoo wake wa rangi nyeupe lakini mwenye kichwa cheusi, amekuwa gumzo la wengi mitaani kwa sababu, kwa kawaida wakazi wa mji huo hawajazoea kuona jambo kama hilo.

Wakazi wa mji huo wanashangaa kama ni mfugo, mazingaombwe au vimbwanga tu vya mjini, kwani hakuna popote bwana huyo huenda, bila kuandamana na kondoo huyo.

Abdurahman Mohamed, amekuwa akionekana ameandamana hapa kwa hapa na kondoo wake huyo mwenye umri wa takriban miezi mitatu, hata anapokuwa kwenye viwanja mbalimbali akitazama mpira.

Lakini ukisikia akieleza ni kwa nini haaachani na myama huyo mchanga, hata wewe msikilizaji labda utamuonea huruma Abdulrahman.

"Mtoto wangu aliaga dunia. Mimi sina mtoto. Kwa hivyo namchukulia huyu kondoo kama mtoto wangu," alikiambia kituo kimoja cha habari nchini Kenya.

Lakini bado kuna baadhi ya watu wanaosema haya ni mazingaombwe na kwamba bwana huyo labda anashiriki ushirikiana.

"Wengine wanasema mimi ni mchawi lakini hayo si kweli," alisema Abdurahman.

Aliongeza kwamba kondoo huyo si wa kawaida kwa sababu yeye hula chakula kama bianadamu.

"Hula Mandazi, hunywa chai, hula Chapati, sima, sukuma wiki zilizopikwa, na hata githeri. Kulinaga na mwenye mnayama huyo, Ajabu hata zaidi ni kwamba anapenda sana kaimati na sambusa za nyama,' aliongeza.

Isitoshe, kwa mujibu wa majirani wa Abdurahman, yeye pia hunywa kahawa tungu. maajabu haya.

Tutoke huko Kenya ambako kondoo wanakunyawa kahawa tungu turejee Marekani lakini tusalie kwa masuala ya wanyama.

Wakazi wa mji wa Paterson jimbo la New Jersey, walipigwa na butwaa siku ya Ijumaa walipowaona darzeni kadhaa za farasi waliokuwa wakikimbia huku na huko na kusababisha wasiwasi mkubwa, hususan kwa sababu, kwa mujibu wa polisi, hawakujulikana walikuwa wametoka wapi, na wala wanyewe walikuwa ni kina nani.

Msemaji wa polisi aliliambia shirika la habari la UPI kwamba kufikia Jumamosi Asubuhi, bado walikuwa wanafukuzana na farasi hao kwenye mitaa ya Paterson, na wakatoa wito wa dharura kwa wamiliki wa farasi hao kujitokeza na kuwachukua ili kuepusha uwezekano wa taharuki kwa wakazi ambao wameendelea kujifungia ndani ya nyumba wakihofia usalama wao.

Cha ajabu hata zaidi msikilizaji ni kwamba, Kwa mujibu wa shirika hilo la habari, farasi hao waliokuwa na ghadhabu, walikuwa wa rangi moja na wote walionekana kuwa kama wa umri sawa.

Tumalizie safari yetu kwenye jimbo la Texas, Marekani. Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 84, ambaye alikuwa akitarajia kuhitimu kutoka shule ya upili mwaka wa 1954, amehitimu wiki hii na kupewa cheti chake rasmi.

Lazima unajiuliza ilikuwajee?

Basi tega sikio.

Paul Markey hakuhitimu mwaka wa 1954 kwa sababu alijiunga na jeshi na kwenda kwa vita vya Korea, mwaka mmoja kabla ya tarehe iliyokuwa imewekwa ya kuhitimu.

Lakini hata ingawa ni zaidi ya miaka 60 tangu arejee kutoka Korea, bodi ya elimu imesema kwamba, kama ishara ya kuonyesha heshima kwa mzee Markey kwa sababu ya kujitolea kwake, na pia kwa vijana ambao hujiunga na jeshi ili kuipigania nchi yao licha ya malengo yao maishani, ni muhimu kumtunuku mzee huyo cheti cha kuhitimu shule ya sekondari.

Msemaji wa bodi hiyo, Tina Veal-Gooch, alisema jimbo la Texas litaendelea kuwapa heshima ifaayo watu wote waliohudumu kwenye jeshi.

Akizungumza baada ya kupata cheti hicho, pamoja na kwelezea fahari yake kwa kuhitimu shule ya sekondari, Markey alisema:

"Ninyi vijana ambao mnatazama tukio hili. Nendeni shule na msalie kwa shule."

Kwli dunia imejaa vijimambo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG