Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:33

Al-Shabab yatishia mashambulizi zaidi Kenya


Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakimsaidia mama kutafuta mwili wa mwanawe
Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakimsaidia mama kutafuta mwili wa mwanawe

Kundi la kigaidi la Somalia al-Shabab limeonya kuwa liatafanya mashambulizi zaidi nchini Kenya kama yale ya chuo kikuu cha Garissa ambayo yaliuwa watu 148 April 2.

"Miji ya Kenya itageuka rangi nyekundu kwa damu," limesema kundi hilo, kulingana na shirika la SITE ambalo linafuatilia habari za kipelelezi.

Magaidi hao walisema wamesema shambulizi la Garissa ilikuwa ni kisasi kwa mauaji yaliyofanywa na majeshi ya Kenya wakati yakipigana na waasi hao nchini Somalia.

"Hakuna kiwango chochote cha hatua za kiusalama ambazo zitahakikisha usalama wenu, au kuepusha shambulizi jingine au kuzuia umwagaji damu mwingine," imesema al-Shabab.

Kufuatia vitisho hivyo vya magaidi hao, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wanamgambo hao wa al-Shabab.

Katika hotuba ya televisheni kwa taifa, Kenyatta alisema utawala wake "utajibu kwa ukali kabisa inavyowezekana" kufuatia shambulizi la Garissa ambalo lilitokea April 2 watu wanne wenye bunduki walipoingia katika majengo ya chuo hicho na kuanza kushambulia wanafunzi kwa bunduki.

Miili ya wengi wa wanafunzi wa waliouawa Garissa imesafirishwa kwenda Nairobi ambako ndugu wamekusanyika kuona na kutambua maiti.

XS
SM
MD
LG