Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:05

Kenya yaimarisha usalama baada ya shambulizi la Garissa


Mwanajeshi wa KDF nchini Kenya akiwa kwenye operesheni baada ya mashambulizi mjini Garissa.
Mwanajeshi wa KDF nchini Kenya akiwa kwenye operesheni baada ya mashambulizi mjini Garissa.

Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, Joseph Nkaissery amewaambia waandishi wa habari Alhamisi usiku mjini Garissa kwamba operesheni iliyoanza mara tu baada ya shambulizi kutokea mjini humo imemalizika.

Mkuu wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet, ametoa amri ya kutotoka nje wakati wa usiku katika kaunti nne za mashariki, ikiwemo Garissa. Amri hiyo inatarajiwa kudumu kwa takriban wiki mbili ikiwa mojawapo ya hatua za kuimarisha usalama.

Wanafunzi wakitoka njee ya chuo kikuu cha Garisa
Wanafunzi wakitoka njee ya chuo kikuu cha Garisa

Shambulizi la Alhamisi lilikuwa na mauaji makubwa kuliko lile la mwaka wa 2013 kwenye eneo la maduka ya kifahari ya Westgate mall mjini Nairobi, ambapo wanagambo wa Al-Shabaab waliokuwa na silaha waliwaua takriban watu 67 katika muda wa siku kadhaa.

Kundi hilo la wanamgambo linaloaminika kuwa na makao yake nchini Somali, limedai kuhusika na shambulizi hilo ambalo lilianza muda mfupi kabla ya alfajiri katika chuo kikuu cha Moi , tawi la Garissa.

Maafisa wa usalama wanasema washambulizi waliokuwa na silaha na silaha walivamia lango la chuo hicho na kuua walinzi wawili, kabla ya kuzingira mabweni na kuanza kuwafiatulia risasi wanafunzi huku wakiwashikilia wengine mateka.

Kifaru cha jeshi la Kenya mjini Garissa
Kifaru cha jeshi la Kenya mjini Garissa

Kwa siku yote ya Alhamisi, Jeshi la kenya lilipambana na wanamgambo hao huku maafisa wakisema washambuliaji wanne waliuawa na mmoja kukamatwa katika operesheni hiyo.

Mbunge wa Garissa, Aden Duale, amesema Kenya itaendelea kupambana na vikundi vyote vya kigaidi. Kwenye hotuba yake kwa taifa mapema jana, rais Uhuru Kenyatta alitoa rambi rambi zake kwa familia za waathiriwa huku akiwasihi wakenya kuwa watulivu.

Rais pia ametangaza kwamba ataharakisha mafunzo ya polisi elfu kumi wa ziada, akisema nchi imepata hasara isiyo faa kutokana na uhaba wa maafisa wa usalama.

Maafisa wa usalama nchini Kenya wamemtaja kamanda wa kundi la Al-shabaab, Mohammed Mohamud aliekuwa wakati mmoja mwalimu katika eneo hilo, kuwa mhusika mkuu kwenye mashambulizi hayo.

Maelezo mafupi ya kiusalama ambayo VOA imeyaona yanasema Mohamud ambaye pia anajulikana kama Gamadhere alikuwa pia mwalimu wa madrassa mjini Garrisa kabla ya kujiunga na kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab.

XS
SM
MD
LG